31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

RC Amour: Rais Samia hahusiki na sadaka ya Sh 5,000 Pemba, ni upotoshaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MKUU wa Mkoa Kusini Pemba, Amour Hamad Salehe, amekanusha taarifa za uzushi zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba, Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa sadaka ya Sh 5,000.

RC Amour ametoa kanusho hilo leo Aprili 6, 2024 Kusini Pemba, Zanzibar ambapo amesela kuwa taarifa hizo ni uzushi na upotoshaji kwa sababu zoezi hilo halihusiani kabisa na Rais Samia kama inavyopotoshwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna mfanyabiashara mmoja amekuwa na utamaduni zaidi ya miaka sita wa kutoa sadaka kwa watoto mayatima kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kwa awamu ya kwanza zoezi la utoaji sadaka lilifanyika kwa ufanisi mkubwa.

“Awamu ya pili wananchi walipeana taarifa iliyohamasisha wananchi kufika kwa wingi. Waliokuwapo kwenye mpango walipata sadaka kama ilivyopangwa. Kwa ubinadamu wake wote waliokuwa nje ya mpango walipewa kila mmoja Sh 5,000 kama nauli ya kurejea nyumbani na sio sadaka,” Alisema RC Amour.

Aidha, katika hatua nyingine, mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa jina la Abas Haji anayemiliki hoteli kwenye eneo la Mgogoni Pemba, alisema; “Msaada huu sio kutoka kwa Mama Samia wala Ikulu au watu wengine. Msaada huu ni mimi kama mimi na familia yangu,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles