31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Rayvanny awa kivutio uzinduzi wa ‘Vuna Deile’

Na Mwandishi Wetu 

Msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, amekuwa kivutio katika uzinduzi wa Promosheni ya ‘Vuna Deile’ iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.


Rayvanny alivutia wageni waalikwa walioudhuria uzinduzi huo kutokana na kuimba nyimbo mbalimbali zilizofanya vizuri ndani nan je ya Tanzania.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rayvanny amesema ni mwanzo mzuri kuelekea katika sikuu ya krismas ambapo watu watajipatia pesa kwa kucheza bahati nasibu hiyo.

“Kila Mtanzania ana nafasi ya kutimiza ndoto ya kumiliki gari kwa kucheza Vuna Deile, mchezo huu hauihitaji nguvu ni kuweka 1000 tu na utaweza kumiliki gari mpya na pia kuvuna mamilioni ya fedha kila siku,’ amesema.

Mratibu wa promosheni hiyo, Nassim Alla, amesema mchezo huo wa bahati nasibu una lengo la kubadilisha maisha ya watanzania wote.

Amesema kila Mtanzania ana nafasi ya kutimiza ndoto zake kwa kucheza Vuna Deile na mchezo huo hauhitaji utaalamu wa aina yoyote zaidi ya kuweka sh. 1,000 tu na utaweza kumiliki gari mpyaa na pia kuvuna mamilioni kila siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles