25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia: Uwanja wa Majaliwa utakuwa chachu katika michezo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa wilaya ya Ruangwa  kwa ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua uwanja wa Majaliwa   katika halmashuri  ya Ruangwa mkoa wa Lindi, Septemba 11, 2022. Kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab  Telack na kulia  kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Dkt. Theobald Sabi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Samia amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo utakuwa chachu katika kukuza sekta ya michezo nchini,

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 11, 2022) alipompigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa uwanja huo, katika halmashuri  ya Ruangwa mkoa wa Lindi,

“Nawapongeza pia kwa sherehe nzuri ya kuzindua uwanja wa mpira wa miguu wa Majaliwa, uwanja huo pia utatumika kwa ajili ya mazoezi kwa timu zetu.”

Awali, akizungumza na Wana-Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa amewashukuru wananchi hao kwa kuamua kuchangia shilingi 20 katika kila kilo moja ya mazao wanayoyauza ili kufanikisha ujenzi wa uwanja huo.

“Natambua mchakato wa ujenzi wa uwanja huu umetokana na mawazo yenu na matamanio yenu,  hivyo mkaamua kutekeleza ili tuwe na uwanja huu. Maamuzi yenu ya kuchangia mlicho nacho yametufikisha hapa. Hongereni sana,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua uwanja wa Majaliwa katika halmashuri  ya Ruangwa mkoa wa Lindi, Septemba 11, 2022. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Aidha, Majaliwa amesema kwa ridhaa ya wakazi wa Ruangwa ambao wameridhia kuendelea kuboresha uwanja huo, msimu ujao wa ligi yatawekwa ili kuwezesha sehemu ya mashabiki kukaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles