24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia atoa pole kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Watanzania wote waliofikwa na athari ya mafuriko katika maeneo kadhaa kama vile Rufiji, Morogoro na mkoani Arusha, akisema serikali yake imeendelea kuchukua hatua kadhaa kukabiliana na hali hizo ikiwa ni pamoja na kupeleka misaada ya chakula na dawa.

Rais Samia ametoa pole hizo leo Aprili 12, 2024 mkoani Arusha wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, ambapo pia ametoa pole kufuatia ajali ya gari ya wanafunzi iliyotokea jijini Arusha na kusababisha vifo vya wanafunzi kadhaa kutokana na uzembe wa dereva wa basi hilo.

Amesema Serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu ya mafuriko hayo.

“Baada ya mvua hizi na hali ya kawaida kurejea, serikali itafanya uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi za mafuriko kwenye maeneo hayo ili tuweze kuchukua hatua zitakazoondoa tatizo hili kwa muda mrefu.

“Niwaombe wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na watendaji wa serikali kwenye maeneo yao. Pia niwaase wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pindi wanapofika sehemu zenye maji yanayotembea iwe wanapita kwa miguu au kwenye magari ili kuepusha athari zozote zinazoweza kusababisha vifo kwa wananchi wetu,” amesema Dk. Samia.

Aidha, Dk. Samia aliwataka Watanzania kuendeleza utamaduni kutoa misaada kwa wahitaji, sambamba na viongozi wa serikali kutumia nafasi zao kwenye majukwaa kuunganisha wananchi na kulisemea ili wananchi wawaelewe na kupata faraja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles