27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini kikaangoni

  • Zuma agoma kuhojiwa tena na tume

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

TAASISI ya kupamba na rushwa  ya Afrika Kusini imesema Rais Cyril Ramaphosa alisema uongo juu ya kiasi cha rand 500,000 ($35,900) takribani shilingi za kitanzania  milioni 83

kilichochangwa na yeye kupokea kwa ajili ya kampeni zake za kuongoza chama cha African National Congress (ANC).

Ramaphosa, ambaye alichukua nafasi ya Rais wa zamani Jacob Zuma mwaka jana na baadae kushinda uchaguzi wa urais na hata  kuapa kupambana na rushwa, alikana kufahamu juu ya mchango huo wakati alipoulizwa na Bunge mwezi Novemba.

Awali Ramaphosa aliwaambia wabunge kuwa malipo hayo yalikuwa ni kwa ajili ya mwanae wa kiume, Andile ambaye alilipwa kwa kazi ya ushauri alioutoa kwenye kampuni ya Bosasa, ambayo sasa inafahamika kama African Global Operations.

Baadae alikiri kuwa mchango huo ulikuwa ni kwa ajili ya kampeni zake za kuwa kiongozi wa ANC.

Mkuu wa Taasisi hiyo ya Kupambana na Rushwa,  Busisiwe Mkhwebane, ambaye anachunguza tuhuma zinazodaiwa kufanywa na viongozi wa serikali, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Ramaphosa alikuwa amevunja Katiba  na kanuni za utendaji wa maadili katika jibu lake hilo kwa Bunge.

Katika ripoti iliyotolewa jana, Mkhwebane  alisema; ” Ingawa Rais Ramaphosa anaweza kuwa na haki ya kurekebisha taarifa ya awali kwa taarifa yenye kosa au ambayo haijakamilika, lakini alipotosha Bunge, “.

Alisema Rais alitakiwa kujipa muda yeye mwenyewe kuchunguza kwa ajili ya kutoa majibu sahihi kabla ya kujibu swali kutoka kwa kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani cha Democratic Alliance, Mmusi Maimane.

“Kwa hiyo nimebaini kuwa kitendo cha Ramaphosa …ingawa kinaonekana ni cha nia njema, lakini ni kinyume na ofisi yake “.

Pia ripoti hiyo imebaini kuwa njia ambayo michango hiyo ilipita kwenye akaunti mbalimbali ikiwamo ile ya kampeni ya Ramaphosa, imeacha shaka ya kuwapo kwa fedha chafu.

Tayari Mkhwebane amewasilisha ripoti hiyo kwenye Kamati ya Bunge ya Maadili, ambayo huenda ikachunguza zaidi.

“Watakachobaini ndicho kitakachoonyesha njia ya nini kitatokea baada ya hapo, lakini hii bado haiwazuii wabunge kupeleka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye kwa spika,”  aliongeza.

 “Si kwamba hicho ndicho kitatokea lakini inaweza kuwa njia mojawapo kwa sasa.” Alisema

ZUMA AGOMA KUHOJIWA TENA

Wakati huo huo  Wakili wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ameiambia tume inayochunguza madai ya ufisadi dhidi ya kiongozi huyo kwamba mteja wake hataweza kushiriki tena mahojiano na tume hiyo kwa sababu anaamini kuwa hatendewi haki kwenye mahojiano hayo.

Wakili huyo  Muzi Sikhakhane aliiambia tume hiyo ya uchunguzi jana kuwa  hawataendelea kushiriki vikao vya uchunguzi, kwani Zuma amekuwa muhanga wa maswali ya kuchafua na kuudhi.

Zuma alikuwa anatarajiwa kufika katika tume hiyo jana kwa ajili ya kuendelea na mahojiano hayo, akiwa tayari ameshahudhuria mengine katika siku tatu zilizopita na  kutoa ushahidi, kabla ya mawakili wake kuomba kuahirishwa kwa mahojiano hayo.

Uchunguzi huo, ambao Zuma alikubali kuunda katika wiki za mwisho za utawala wake, unaangazia madai ya ufisadi pamoja na matumizi ya ushawishi ambayo yalikuwapo katika utawala wake wote wa miaka tisa madarakani.

Mapema wiki hii baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza mbele ya timu inayochunguza tuhuma hizo Zuma alimwambia jaji anayeongoza uchunguzi  huo kwamba tuhuma hizo zilikuwa ni njama za kumwondoa kwenye ulingo wa siasa.

Zaidi alizishutumu taasisi za kiusalama za kigeni, ambazo hakuzitaja  kuwa zilikuwa nyuma ya mpango huo uliosukwa kwa miongo kumwondoa madarakani.

Tuhuma dhidi ya Zuma ni zile zinazolenga uhusiano wake wa shaka na familia ya Gupta ambayo inashutumiwa kushawishi uteuzi wa baraza la mawaziri na zaidi kushinda tenda zenye faida kubwa kwa njia ya rushwa katika serikali yake.

Pia alikuwa anatuhumiwa kuchukua rushwa kutoka kampuni ya Bosasa, inayoendeshwa na familia ya Watson.

Hata hivyo Zuma alipinga tuhuma kwamba aliruhusu serikali ishikwe na familia ya Gupta, au kuuza nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,406FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles