Rais Magufuli auguliwa na mama yake mzazi

0
1252

iNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amemjulia hali mama yake mzazi, Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam kwa muda wa miezi mitatu sasa baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kwamba baada ya Rais kumjulia hali mama yake pia aliongoza maombi ya kumwombea pamoja na watu wote wanaokabiliwa na maradhi na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2019.

Pia aliwashukuru madaktari na wauguzi wanaomuhudumia mama yake na wagonjwa wengine nchini na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu heri na fanaka katika majukumu yao ya kunusuru maisha ya watu.

Awali Rais Magufuli, aliungana na waumini wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam kuadhimisha sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Joseph.

Misa Takatifu ya kuadhimisha sherehe hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi, Padre Bathlomeo Bachoo ambaye alisisitiza umuhimu wa jamii kujenga familia bora, inayochapa kazi na inayomcha Mwenyezi Mungu.

Padre Bachoo pia amempongeza, Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kutanzua sintofahamu kuhusu mafao ya wastaafu na ametoa wito kwa familia zitakazonufaika na uamuzi huo kutumia mafao hayo kujenga umoja na kuimarisha familia zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here