RAIS MAGUFULI ATUMA RAMBIRAMBI VIFO VYA WATU 26 PWANI

0
709

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli, ametuma salam za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, EvaristNdikilo kutokana na vifo vya watu 26 vilivyotokea jana katika ajali baada ya basi dogo kugongana na lori lililokuwa limebeba chumvi katika Kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Katika salam zake Rais Magufuli amesema amesikitishwa na taarifa ya vifo hivyo n akuongeza kuwa tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvukazi ya Taifa.

“Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu waliowategemea,” amesema Rais Magufuli katika taarifa yake.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyoshughulikia usalama wa barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili huku akiwaombea majeruhi wa ajali hiyo wapone haraka na kuungana na familia zao na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here