QATAR YAPEWA SAA 48 ZAIDI KUTEKELEZA MASHARTI YA NCHI ZA KIARABU

0
800

Saudi Arabia na nchi tatu za kiarabu zimeongeza muda kwa nchi ya Qatar, kutimiza masharti iliyopewa la sivyo iwekewe vikwazo zaidi baada ya saa 48.

Tarehe ya mwisho ya kuitaka Qatar kukubali masharti 13, ikiwemo ya kukifunga kituo cha Al Jazeera ilimalizika siku ya Jumapili.

Taifa hilo la ghuba linasema kuwa litajibu kupitia barua ambayo itawasilishwa kwa Kuwait leo Jumatatu.

Qatar inakana madai kutoka kwa majirani zake kuwa inafadhili itikadi kali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here