24.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 30, 2022

Contact us: [email protected]

“Polisi wamerejesha amani, Panya Road wametokomea wote”-Wananchi

*Amani imetawala, hakuna anayeibiwa hata kijiko

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameipongeza Serikali kupitia jeshi la polisi kwa namna ilivyofanikiwa kukomesha makundi ya vijana wahalifu maarufu kama ‘Panya Road’ waliokuwa wakivamia na kupora vitu katika maeneo mbalimbali.

Wakizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatatu Oktoba 3, 2022 wakazi hao wamesema kuwa kwasasa wana amani kwani jeshi la polisi limefanya kazi kubwa ambapo hakuna anayeibiwa hata kijiko.

Bushiri Ally Napwil.

Bushiri Ally Napwili ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyembwera kata ya Tandika jijini Dar es Salaam ambaye amekiri kuwa amani imerejea mtaani.

“Tukianza kuzungumzia namna hawa vijana wa panya road walivyokuwa wanasumbua sababu wanaanzia huku chini, ilikuwa ni shida sana na amani tulikuwa hatuna, lakini baada ya operesheni ya kitaifa, mimi nipongeze jeshi la polisi kuanzia kwa IGP Wambura(Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillius Wambura), Rais wetu Samia Suluhu Hassan, sasahivi wananchi tunaishi kwa amani na utulivua mbao ulikuwa umekosekana sasahivi umerejea.

“Na hivi ndivyo serikali inavyotakiwa kuwa kwani haiwezekani wananchi wasiheshimu na ndiyo maana imeweza kudhibiti vijana hawa wa panya road na hata waliobakia wamekimbia,” amesema Bushiri na kuongeza kuwa:

“Mtaani kwangu nilipata adha hii kwa vijana wawili kukumbwa na hii oparesheni ya kitaifa, hii imesaidia mtaa umekuwa tulivu na hata yale makundi na sura ambazo zilikuwa zinatoka Keko, Chanika, Mbagana na sehemu nyingine zote zimetokomea sababu walikuwa wakiwafuata washirika wao ambao sasahivi hawapo na sidhani kama kuna mtu ambaye angeweza kukaribia hatari hiyo.

“Kwa hiyo mimi naanza kujipongeza mwenyewe lakini pia naipongeza serikali yetu, kwani sasahivi unauwezo wa kuwambia walinzi wetu wa kikosi cha ulinzi shirikishi wakapumzika hata siku tatu bila kufanya kazi na amani ikawa imepatikana kwani hakuna mtu anayevunjiwa, kukabwa wala kuchukuliwa kijiko, kwani maisha yamerudi kama zamani, hivyo polisi wamefanya kazi nzuri sana,” amesema Bushiri.

Upande wake, William Kessy ambaye ni mkazi wa Buza na mjumbe wa shina namba 6, amesema kuwa kuna kila sababu ya kupongezwa kwa jeshi la polisi kwani limefanya kazi kubwa ya kurejesha amani.

William Kessy

“Tangu wiki iliyopita ambapo jeshi la polisi lilipita na kufanya kazi kubwa na tunaamini kuwa hali itaendelea hivi,” amesema Kessy.

Nae, Habiba Mohamed mkazi wa Buza kwa Lulenge amesema mbali na kupongeza jeshi la polisi pia ameomba liendelee na mpango huo wa kuwadhibiti panya road kwani wamefanya unyama ambao umeumiza watu wengi.

Habiba Mohamed.

“Tunaomba polisi iendelee kuwadhibiti hawa panya road kwani mambo wanayofanya ni uuaji na tunashangaa baadhi ya wazazi kuwatetea watoto wao, hivyo me naomba polisi waendelee kabisa ili tuishi kwa amani kwani wanachofanya ni unyama ambao unaumiza wananchi na kusababishia ulemavu ukiwamo umauti kwa watu.

“Kwani hawa ni wauaji na kama isingekuwa hivyo basi wasingekuwa na haja ya kukata mapanga watu kichwani, hivyo polisi wamefanya kazi nzuri tunaomba iendelee,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles