25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Kagera wakamata pikipiki 157

Na Renatha Kipaka, Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera kwa kushirikiana na jeshi la ulinzi nchini Burundi wamekamata pikipiki 157 zilizokuwa zimeibwa na bunduki 11 zilizokuwa zikitumika kwenye vitendo vya uhalifu ndani ya kipindi cha Septemba hadi Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Kagera, ACP Brasius Chatanda wakati alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari na kusema kuwa matukio ya wizi wa pikipiki yamekuwa yakiongezeka na kuwataka madereva bodaboda kuchukua tahadhari wawapo barabarani.

“Tunaweza kuona ni kwa kiwango gani matukio ya wizi wa pikipiki yalivyo makubwa sasa bodaboda wanapokuwa barabarani wachukue tahadhari hatujui hizi pikipiki zilipotoka hawa walioibiwa wako salama, hawakufa, hawakujeruhiwa,” amesema Chatanda.

Aidha, amewasihi wote walioibiwa wafike kituo kikuu cha polisi Bukoba kwa ajili ya kuangalia iwapo kuna pikipiki zao kwenye hizo zilizokamatwa.

Kwa upande wake, John Kweyamba ambae anafanya kazi ya bodaboda mjini Bukoba amesema kwa jinsi hali ilivyo wanatakiwa kuchukua tahadhari hasa nyakati za usiku ili kuepuka kuibiwa pikipiki.

Aidha, ACP Chatanda ameongeza kuwa katika msako huo jumla ya silaha 11 zikiwamo AK 47 mbili zimekamatwa ndani ya kipindi cha mwezi Septemba hadi sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles