28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Pinda ataka mabadiliko NHC

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda amefanya ziara Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) na kulitaka kufanya mabadiliko makubwa katika nyanja zote za utoaji huduma kwa watumishi wa NHC ili waweze kuleta tija kubwa kwa shirika na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda.

Akizungumza Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam Pinda amesema kuwa amefanya ziara hiyo ili kufahamu kazi zinazofanywa na NHC na kuzungumza na wafanyakazi wa makao makuu kwa niaba wafanyakazi wote wa shirika.

“Nichukue nafasi hii kuwapongezeni kwa kazi kubwa mnazozifanya kwa maendeleo ya Taifa, tunataka mabadiliko makubwa ya utoaji huduma ndani ya NHC kwa kila mmoja kufanya kazi apaswayo sisi kama Serikali tutawaunga mkono kama mlezi wenu,” amesema Pinda.

Aidha, ametaka kuongezwa kasi ya kudai kodi kwa wadaiwa sugu wa shirika hilo na kwa zile taasisi za Serikali ambazo nazo ni wadaiwa sugu orodha yao iwasilishwe Wizara ya Ardhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles