23.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda ajitosa kuinua lishe bora Kagera

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo  r Pinda, amesema asasi zisizo za serikali zitachochea vikubwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini endapo zitahamasisha  ushiriki wa vijana na wanawake kwenye sekta  za kilimo, uvuvi na biashara.

Alikuwa akizungumza na ujumbe wa Agri-Thamani Foundation ya Mkoa wa Kagera uliomtembelea nyumbani kwake  Pugu, Dar es Salaam jana  kumshukuru kwa kuwa mlezi wa asasi hiyo.

Pinda alisema thamani na nguvu asasi zizizo za serikali duniani kote ni katika kusaidiana na serikali  kuneemesha  maendeleo ya wananchi.

Aliahidi kuitumia asasi hiyo kwa ajili ya kuinua lishe bora mkoani Kagera.

“Mimi pia ni mkulima na nina uzoefu wa muda mrefu katika kilimo. Kwa sababu hii naamini nitaweza kuchangia vema katika kuiongoza taasisi hii kufikia malengo yake  na kwa kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano kujenga uchumi wa kati na viwanda.

“Ni matumaini yangu tutashirikiana kuinua lishe Mkoa wa Kagera. La muhimu ni ushirikiano na uaminifu wa hali ya juu,” alisema Pinda.

Alitumia fursa hiyo kuwaeleza Watanzania kwamba ili asasi zisizo za serikali zifikie malengo yake ni lazima zihamasishe ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta za kilimo, uvuvi na biashara.

Alisema tatizo la unyafuzi linasababishwa na kukosekana lishe bora, kwa sababu  lishe bora ni muhimu kwa afya njema na kumwezesha mtu kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Pinda aliahidi kwamba   atahakikisha asasi hiyo inashirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na taasisi nyingine za afya ndani na nje ya nchi.

Alisema hatua hiyo itasaidia kufikisha kwa haraka elimu ya lishe kwa walengwa kwa usahihi, hasa makundi ya vijana na wanawake wa Mkoa wa Kagera kutambua umuhimu wa lishe na afya bora katika juhudi za kuleta maendeleo.

Naye Mwenyekiti na mwanzilishi wa asasi hiyo, Neema Lugangira, alisema sehemu pekee ambayo lishe bora inaweza kupatikana ni kupitia kilimo, ufugaji na uvuvi.

“Ili taifa liwe endelevu linahitaji kuwa na wananchi wenye afya nzuri,  mwili na  akili pamoja na nguvu ya kufanya kazi.

“Nitoe wito kwa vijana na wanawake wa Kagera kutumia fursa hii kwa kushirikiana na taasisi yetu katika kutokomeza tatizo la utapiamlo na magonjwa mengine ya lishe mkoani Kagera,” alisema Lugangira.

Alisema Tanzania inategemea wananchi wake kutumia fursa zilizopo kuendelea na kwa kutimiza hilo, vijana wanategemewa kwa kiasi kikubwa.

“Ni matumaini yangu wananchi wa Kagera wataweza kuondokana na umaskini, kuimarisha hali ya lishe  na ushiriki wenu katika mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na uvuvi kuimarika,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles