28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Pialali awataka mabondia kumpa Mwakinyo heshima yake

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali amewataka mabondia wenzake kuheshimu kiwango alichofikia Hassan Mwakinyo na kupambana kufikia viwango vyake kuliko kutumia muda mwingi kumsema vibaya.

Idd Pialali.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Pialali amesema Mwakinyo ni bondia aliyeipa heshima kubwa Tanzania katika mchezo, hivyo wanatakiwa kujifunza kwake na si kumkebehi kwa maneno.

“Kwa mimi siwezi kumsema vibaya Mwakinyo kwa sababu najua yupo juu yetu na ameiletea heshima Tanzania na mchezo wa ngumi. Tunachotakiwa kufanya kama mabondia ni kumpa heshima yake na kupambana kufika mahali alipo,” amesema Pialali.

Pialali anatarajiwa kupanda ulingoni Septemba Mosi, 2023 kurudiana Mfaume Mfaume kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya pambano lao la Desemba mwaka jana kuvunjika na kukosekana mshindi.

Bondia huyo amesema anajiandaa vizuri kuhakikisha anammaliza mapema akidai mpinzani wake Mfaume amekuwa akiongea sana.

“Mimi huwa sina maneno mengi, mashabiki wangu watarajie burudani ya ngumi na ushindi, Mfaume safari hii hatakuwa na cha kujitetea kwa sababu pambano lililopita hakupatikana mshindi,” ametamba Pialali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles