20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

Pia atwaa taji la Miss Universe kwa utata

piaLOS VEGAS, MAREKANI

MREMBO kutoka nchini Ufilipino, Pia Wurtzbach, amefanikiwa kutwaa taji la Miss Universe Pageant, baada ya kumshinda mpinzani wake kutoka nchini Colombia, Ariadna Arevalo, kwa utatanishi.

Katika hafla hiyo ambayo ilifanyika kwenye ukumbi wa Planet Hollywood Resort, nchini Marekani, iliwaacha watu midomo wazi baada ya mtangazaji, Steve Harvey, kufanya makosa wakati wa kumtangaza mshindi wa taji hilo.

Harvey alijikuta akilitaja jina la mrembo kutoka nchini Colombia, Ariadna badala ya Pia wa nchini Ufilipino.

Baada ya kulitaja jina hilo mashabiki wa mrembo huo walishangilia kwa furaha kubwa, lakini baada ya dakika chache mtangazaji huyo alirudi kwenye jukwaa na kuomba radhi kwa kudai alikosea na kisha kuanza kumtangaza Pia ni mshindi kutoka nchini Ufilipino.

“Siwezi kuamini kilichotokea, nilijikuta nikitaja jina la Ariadna badala ya Pia, nimefanya kosa kubwa sana mbele ya maelfu ya watu lakini sina jinsi zaidi ya kuwaomba radhi watazamaji wote,” alisema  Harvey.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles