23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Philips kutengeza CT Scan Muhimbili

mri--1Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  umesema wakati wowote   Kampuni ya Philips itazitengeza mashine za CT-Scan na MRI  ziweze kutoa huduma kwa wagonjwa.

Umeyasema hayo siku moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kutembelea hospitali hiyo na kumng’oa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto

Kaimu Mkurugenzi mpya wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Mseru, pia amewahimiza wafanyakazi wa hospitali hiyo kuzingatia nidhamu ya kazi kila mmoja kulingana na maelezo aliyopewa katika mkataba wake wa kazi.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa MNH, Aminiel Eligaesha, alikuwa akizungumza na  MTANZANIA baada ya kumalizika  kikao kati ya wafanyakazi na uongozi wa hospitali hiyo.

Alisema Profesa Mseru   amekwisha kuanza mazungumzo na kampuni ya Philips   kutengeneza mashine za CT Scan na MRI ambazo zimeharibika.

“Kaimu Mkurugenzi jana alikuja   kujitambulisha ili kufahamiana lakini kikubwa ni   amehimiza ushirikiano na nidhamu ya kazi kwa kila mfanyakazi,” alisema.

Awali akizungumza na MTANZANIA, mgonjwa mmoja Jackson Makenge alisema anamshukuru Mungu kwa kutembelewa na Rais na kumpatiwa msaada wa matibabu.

Makenge ni mmoja wa wagonjwa aliyepata bahati ya kuzungumza na Rais Dk. Magufuli    ambaye amemgharamia kupatiwa vipimo nje ya hospitali hiyo.

“Namshukuru Rais Magufuli kwa ziara yake na kitendo  cha kutukumbuka wagonjwa, lakini ni wakati sasa kwa kila mmoja kuwajibika   bila kusubiri kusimamiwa,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kilolomo, alisema ziara ya  Rais Dk. Magufuli   itasaidia kutatuliwa  changamoto zinazowakabili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles