26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Pampu za kukamulia maziwa watoto hatari

Hassan Daud na Mashirika ya Habari duniani

PAMOJA na  kwamba imekuwa ni kawaida kwa akina mama wengi wa sasa hasa wale wanaopenda kwenda na wakati kutumia njia za kisasa kama ile ya pampu kuvuta maziwa kwa ajili ya kuwapa watoto wao, imebainika  njia hiyo ni hatari kwa afya za watoto.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Manitoba, Canada, na kuchapishwa katika Jarida la Cell Host & Microbe, umeeleza kuwa mtoto kunyonya maziwa kupitia pampu hizo huwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa pumu.

“Watafiti walisema pampu zinazotumika kunyonyesha watoto ni rahisi kubeba bakteria wanaoishi katika mazingira yanayomzunguka, tofauti na wale wanaotumia chuchu za mama zao,” alisema Dk. Shirin Moossavi aliyeongoza utafiti huo.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Daily Mail la Uingereza, msomi huyo aliongeza kuwa si tu pampu hizo huweza kumsababishia mtoto ugonjwa huo wa pumu, pia anaweza kuwa na tatizo la uzito au mzio (allergy).

Kufanikisha utafiti wake, Chuo Kikuu cha Manitoba kiliwafuatilia akina mama 393 waliojifungua miezi minne iliyopita. Majibu yalionesha kuwa maziwa ya wengi waliokuwa wakitumia pampu yalikuwa na bakteria aina ya Stenotrophomonas.

“Bakteria aina ya Pseudomonadaceae huaribu mfumo wa mkojo na huathiri mfumo wa damu na upumuaji, ambao kwa mtoto huweza kumsababishia pumu hapo baadaye,” ilieleza ripoti ya utafiti huo.

Wakielezea umuhimu wa wazazi kunyonyesha kwa kutumia chuchu zao na si pampu, watafiti hao walisema hiyo huwasaidia watoto wao kupata bakteria wanaofaa kwa ajili ya afya zao.

“Miongoni mwao ni Bifidobacterium, ambao ni bakteria wazuri katika kufanikisha mmeng’enyo wa chakula na humuepusha mtoto na maambukizi ya magonjwa,” alisema Dk. Moossavi.

Akisisitiza hilo la wazazi kunyonyesha watoto kwa kutumia chuchu zao, Moossavi alisema mtoto hupata bakteria waitwao Gut microbiota ambao ni muhimu kwa kinga yake ya mwili.

“Endapo mtoto atawakosa hao Gut microbiota katika hatua za mwanzo za ukuaji wake, baadaye haitashangaza kuwa na magonjwa ya ngozi na pumu,” aliongeza Dk. Moossavi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles