23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

PADRE: WAHUSIKA MAUAJI YA AQUILINA WALIOMBE TAIFA MSAMAHA

Padre wa Parokia ya Yohana Mbatizaji, Kigogo Luhanga anayeongoza misa inayoendelea sasa hivi katika Viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), ya kumuombea Marehemu Aquilina Akwilini, Raymond Manyanga amesema anayehusika kumpiga risasi binti huyo aliombe taifa msamaha kutokana na kitendo hicho.

“Naomba wote tuwe wapatanishi, hili lililotokea limetuumiza tunawaomba wanaohusika hasa wenye madaraka, aliyefanya kitendo hiki akijulikana aliombe taifa msamaha maana Aquilina hawezi tena kurudi,” amesema Padre Manyanga.

Amesema Aquilina ameondoka ghafla, hatukutegemea jambo linloumiza ambapo vyombo vya habari vimeripoti kwamba alipigwa risasi lakini hawezi kulisemea sana hilo na kuongeza kuwa: “kama kweli ndivyo basi tuombe Mungu atuepushe na matukio ya namna hii, maana leo ni Aquilina kesho hatujui nani mwingine.”

“Naomba niseme bila kuwa na kigugumizi, wenye nafasi hii si wengine bali serikali naomba hili watusaidie maana ndiyo waliopewa dhamana, tupo kama vidole hatulingani wote ni watoto wa baba mmoja, nina imani serikali yetu itatupatanisha na kurudi ili tuwe wamoja,” amesema.

Aidha, amesema inasemekana Aquilina amepigwa risasi na risasi haiwezi kwenda yenyewe, imepigwa na mtu ambapo anaamini ni mtu huyo mwenye akili timamu sasa kwanini alipiga ni jambo analojiuliza na kutaka watu kumuomba Mungu atupe hekima, busara na kuvumiliana.

“Tumeishi miaka 50 ya Uhuru sitegemei matukio ya namna hii, tuishi kama watu waliokomaa tuidhihirishie dunia kwamba tumekomaa na tuishi kwa umoja.

“Tusipopatana tutamalizana, tusipokubali kwamba sisi wote ni wana wa Mungu na tutakubali uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu hatutaishi kwa pamoja kama watoto wa Mungu, tumuombe Mwenyezi Mungu tuwe wapatanishi na si wagombanishi,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles