Na Janeth Mushi, Arusha
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Olenasha amepokea mabomba na vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 246.

Mabomba hayo na vifaa hivyo vinatarajiwa kutekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Piyaya, Kisangiro, Masusu, Sale, Olaika, Samunge, Digodigo na Sanjani, wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika katika Ofisi za RUWASA, Ngorongoro Julai 26, 2021, Olenasha ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hilo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngorongoro, Ndirango Laizer na Mwenyekiti wa Halmashauri, Emanuel Shangai.
Wengine ni, Mwenyekiti wa UWT Wilaya, Fatma Ngorisa na Wajumbe wengine wa Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Ngorongoro.
Olenasha amesema kuwa Tangu kuanzishwa kwa RUWASA wilaya ya Ngorongoro ameona kuwa miradi ya maji ikitekelezeka na amesisititiza miradi yote ya maji itekelezwe kwa wakati ili wananchi wapate huduma ya maji.