26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Nyota Simba wahamishia vijembe mitandaoni

Na Winfrida Mtoi

Baada ya kufanikiwa kutetea mataji yao yote mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC), nyota wa kikosi cha Simba  wamekichafua mitandao ya kijamii, huku wakitupa madongo wa wapinzani wao.

Wachezaji hao, wengi wametupia picha wakiwa wamelala na kombe  la ASFC walitwaa jana baada ya kuwafunga watani wao Yanga bao 1-0 katika mchezo wa fainali ulipigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mkoani Kigoma.

Miongoni mwa wachezaji walioandika jumbe mbalimbali katika kurasa zao za instagram ni beki Mohammed Hussein ‘’Shabalala’ambaye ameandika jumbe tofauti zikisema,“Shinda makombe ili usipate tabu ya kujielezea kuwa wewe ni mchezaji mkubwa.

“Lazima nilishikilie kwa mikono miwili kuna mtu anaitwa Deus Kaseke asije kuniibia kombe langu.  Mwenye namba ya daktarin wa mabega anitumie DM,”

Bernard Morrison “Timu kubwa siku zote ina njaa ya makombe.

Meddie Kagere ameweka picha akiwa amesimama na   C.E.O wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez na kuandika kuwa,”Jamani msisahau kuniamsha wakati mkisikia kombe lolote mjini, inauma.

Clatous Chama, ameandika kuwa wenye mji tumefika, tulale sasa hivi au tusubiri kidogo?

”Wakati Simba  inachukua kombe hili mara ya pili mfululizo, kumbuka HD analinyanyua mara ya tatu, kweli si kweli?? Kazi ya mwanaume hatumwi mvulana” ameandika Hassan Dilunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles