24.1 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

NMB yasisistiza taarifa sahihi kwa wateja wake wenye changamoto za biashara

Na Derick Milton, Simiyu

Benki ya NMB imewataka Wafanyabiashara ambao ni wateja wao, wanaopata changamoto kwenye biashara zao kwenda katika benki hiyo na kutoa taarifa kwani taasisi hiyo imekuwa na taratibu za kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba wafanyabishara.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 19, 2022 na Meneja Mwandamizi kitengo cha Biashara NMB, Christopher Mgani, wakati akizungumza na wafanyabiashara zaidi ya 200 wa Mkoa wa Simiyu kwenye Kongamano la Klabu ya Wafanyabiashara ( Business Club).

Mgani amesema NMB baadhi ya wateja wao ambao wamekuwa wakipata mikopo wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali kwenye shughuli zao za kibiashara, ambapo amesema benki hiyo imeweka taratibu za kuweza kutatua changamoto hizo.

Amesema kuwa wafanyabishara ambao wamekopa NMB na wakata changamoto mbalimbali, wanayo nafasi ya kwenda katika benki hiyo na kutoa taarifa za changamoto zao kisha ziweze kutatuliwa.

Amewasisitiza wafanyabiashara pindi wanapopata hali hiyo, wasikimbie na badala yake wanayo nafasi ya kwenda kueleza changamoto zao na kusikilizwa kisha ziweze kutatuliwa.

“Kama benki tumekuwa na utaratibu wa kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwapata wateja wetu hasa wale wenye mikopo, kwanza, tunaweza kupunguza marejesho, tunaweza kuongeza muda wa kurejesha, lakini tunaweza kukuongezea fedha ili tukukwamue kwenye changamoto yako.

“Lakini jambo kubwa la muhimu kama wewe ni mteja wetu ulipata mkopo na ukapata changamoto, njoo tuzungumze …tuletee taarifa lakini changamoto hizo zinatakiwa kuwa za kweli,” amesema Mgani.

Akizungumzia klabu za wafanyabiashara, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Sospter Magesse amesema klabu hizo zimekuwa na tija kubwa kwa benki hata kwa wafanyabiashara wenyewe.

Amesema kuwa kupitia klabu hizo, Benki pamoja na wafanyabiashara ambao ni wateja wao, wamekuwa wakikutana kisha kila upande kueleza changamoto zilizopo na kuweza kuzitatua kwa pamoja.

“Kama benki tunajivunia sana na uwepo wa Klabu za wafanyabiashara kwa muda wa miaka saba sasa, tumekuwa tukiwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali na kuwapa elimu za kibiashara na utunzaji wa fedha,” amesema Magesse.

Mmoja wa wafanyabiashara kutoka mjini Bariadi, Flora Shilingi amesema kuwa kupitia mafunzo ya Klabu za biashara, yamewawezesha kujua kutunza kumbukumbu za mahesabu pamoja na lakini pia umuhimu wa utunzaji pesa benki.

Mwenyekiti wa Klabu ya wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Christopher Muhama amesema kuwa kwa muda wa miaka saba tangu kuwepo wa klabu ya wafanyabiashara NMB mkoa wa Simiyu kumekuwepo na mafaniko makubwa.

Amesema kuwa mafanikio makubwa wamekuwa wakipata mikopo yenye riba nafuu na kwa wakati, huku wakisaidiwa changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye biashara zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles