25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Watendaji wa Sensa watakiwa kufanya kazi kwa bidii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watendaji wa Sensa nchini wamepewa wito kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukamilisha kwa ufanisi wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Augusti 23, 2022.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam Agosti 18, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene katika kikao cha saba cha Kamati Kuu ya Sensa ya Watu na Makazi

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizungumza katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Saalam.

“Baada ya zoezi la sensa ya watu na makazi kuna kazi kubwa ya mchakato lazima tuwe tayari kusimama pamoja na kufanya kazi usiku na mchana ili zoezi liweze kukamilika,” amesema Simbachawene.

Waziri Simbachawene ameipongeza kamati ya Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo kufanikisha maamuzi ya kamati kuu ya Taifa ya Sensa.

“Vilevile napongeza Wizara zote, Wadau wa Maendeleo na Sekta binafsi kwa ushirikiano mkubwa  walioonesha wakati wote wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi,” amesema Simbachawene.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizungumza jambo kabla ya kikao na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk, Alibina Chuwa.

Upoande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Alibina Chuwa amesema kwa wakuu wa kaya ambao hawatakuwa nyumbani wameandaa fomu maalumu ambayo itakuwa na maswali 11 ambayo itasambazwa kwa wakuu wote wa kaya kupitia kwa makarani wao wa sensa.

“Wakuu wa kaya waandike taarifa za watu ambao watakuwa wamelala usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kumrahisishia karani kujaza taarifa kwenye kishikwambi atakapofika kuchukua taarifa,” amesema Dk. Chuwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles