23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

NIMR waanza tafiti tisa za corona

Tunu Nassor Na Christina Gauluhanga -Dar es salaam

TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imeanza kutekeleza tafiti tisa zinazohusu ugonjwa wa homa ya mapafu Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya, alisema tafiti hizo ni pamoja na utafiti juu ya epidemologia na athari katika mwili wa binadamu na kasi ya kusambaa kwa Covid 19 nchini Tanzania.

Alisema utafiti mwingine ni kuhusu tathmini ya uelewa na kiwango cha kutekeleza maelekezo ya kujikinga na virusi vya corona kwa Dar es Salaam na Zanzibar.

“Tunafanya tafiti pia kujua usalama na ufanisi wa NIMRCAF (dawa lishe ya corona ya taasisi hiyo) katika kuongeza uwezo wa mwili kupambana na COVID19,” alisema Profesa Mgaya.

Alisema wanatafiti pia kujua uelewa na mikakati ya kuzuia wagonjwa wenye virusi vya Ukimwi, kisukari, na shinikizo la damu wasiambukizwe COVID19.

Aliongeza pia utafiti mwingine ni juu ya uelewa na mikakati ya kuzuia COVID19 kwa wagonjwa wenye virusi vya ukimwi walioko kwenye hatari ya kupata kisukari na magonjwa sugu.

“Tunatafiti kujua tabia za usafi zinazohusiana na mapambano dhidi ya mlipuko wa COVID19 jijini Dar es Salaam,” alisema Profesa Mgaya.

Alisema wanafuatilia mwenendo wa maambukizi ya COVID19 nchini kwa kutumia hisabati na majaribio ya mshikamano kwa ajili ya ugonjwa huo.

Alisema utafiti mwingine ni kutathmini upatikanaji wa vifaa kinga na utoaji wa huduma za vipimo dhidi ya Covid19 kwenye miji midogo ambayo magari makubwa ya mizigo hupumzika hapa nchini.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,426FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles