26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Nedy Music ajikita kwenye maandamano ya amani ya mtandaoni Nigeria

NA MWANDISHI WETU

NYOTA wa muziki Bongo fleva Tanzania Said Self ‘ Nedy Music,’ amejiunga na maandamano ya EndSARS kupitia mitandao wa kijamii kwa ajili ya kupinga machafuko nchi Nigeria.

Nedy Music aliwahi kushinda tuzo ya AFRIMA 2018, zinazotolewa nchini Nigeria, kipengele cha Chaguo la Mashabiki (African Fans’ Favourite) kupitia nyimbo yake ya Ameni.

Akizungumza na ukurasa huu amesema ameungana na mamilioni ya watu kuandamana ili kupinga ukatili unaofanywa na polisi kwa wananchi wake nchini humo.

“Nimeamua kujiunga na kundi hili la mtandaoni ambalo linapinga ukatili unaofanywa na polisi wa Nigeria kwa wanachi hususan vijana ambao ndio tegemezi la dunia,” alisema Nedy Music.

Aliongeza kuwa yeye kama msanii kioo cha jamii, ataendelea kuungana na mamilioni nchini Nigeria wanaotumia sauti zao na vipaji katika maandamano hayo ya amani yenye kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

Ni wiki tatu sasa zimepita tokea waandamaji wa Nigeria wakitaka kutokuwepo kwa ukatilii wa polisi kwa raia wake (ENDSARS), kumekua na mapolisi wengi wakijihusisha kuwatesa wananchi wa kinigeria na kuwapa mateso makali kwa kipindi.

Nedy Music na wahamasishaji wengine wameingia kwa kishindo katika mitandao ya kijamii huku wakituma picha mbalimbali zenye mabango zikiashiria kwamba iwe mwisho wa ukatili wa polisi kwa wananchi (ENDSARS).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles