25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ndege iliyonunuliwa na Serikali yatua nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamriho (wa nne kushoto), akiongoza na maofisa wa Serikali na maofisa wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft, kukagua moja ya ndege zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamriho (wa nne kushoto), akiongoza na maofisa wa Serikali na maofisa wa Kampuni ya Bombadier
Commercial Aircraft, kukagua moja ya ndege zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam jana.

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

NDEGE mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  Dar es Salaam jana, ikitokea Canada ilikotengenezwa.

Ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 NextGen  ilitua  saa 6.00 mchana  na kisha kupatiwa heshima maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi husika (Water Salute).

Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege hiyo iliegeshwa katika eneo la ndege za jeshi Ukonga (Airwing Ukonga).

Akizungumza baada ya kuwasili

ndege hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.  Leonard Chamriho alisema ndege ya pili itawasili baada ya wiki moja.

“Baada ya kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi yatakayoongozwa na Rais John Magufuli kwa tarehe itakayotangazwa baadaye,”alisema Dk. Chamriho.

Mkataba wa makubaliano ya awali ya ununuzi wa ndege hizo ulitiwa saini Dar es Salaam, Agosti, 2014  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni hiyo ya Bombardier Kanda ya Afrika.

Bombardier ni kampuni pekee duniani inayotengeneza ndege na treni za kisasa kwa pamoja. Makao makuu ya kampuni hiyo yako Montréal, Canada.

ATCL lilianzishwa Machi 11,1977 baada ya kuvunjika kwa lililokuwa Shirika la Ndege la Afrika Mashariki. Kwa sasa shirika hilo lina ndege moja tu ya Dash 8, Q300.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles