26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

NATAMANI WOLPER, HARMONIZE WANGEJUA WANACHOKIJUA FLORA MVUNGI, H. BABA

wolper na harmonize mapenzi

Na RAMADHANI MASENGA

KUNA taarifa kuwa Harmonize na Jackline Wolper wameachana. Kwa baadhi ya watu hii sio taarifa ya kushtua hata kidogo. Hata mimi nilishtuka kidogo tu baada ya taarifa hii. Kwanini?

Kwa sababu mapenzi ya sinema hayana uhai mrefu. Wachunguzi wa maisha ya wasanii wanajuza kuwa mahusiano ya Wolper na Harmonize yalikuja baada ya Wolper kuona hakuna msanii wa kiume aliye ‘single’ na aliyekuwa  katika chati ya juu kwa wakati huo.

Ukiangalia Diamond alikuwa busy na Zari wake, Ali Kiba na Jokate, Mr Blue kaoa na katulia huku Rayvanny hakuwa anasomeka. Nani angekuwa naye kama sio Harmonize ambaye alikuwa single na  mwingi wa matongotongo ya Mtwara?

Baadhi tulijua Harmonize ni ngumu sana kuwa na Wolper. Harmonzie ni kijana makini mwenye kutaka majaliwa mema ya familia yake.

Harmonize hajatoka katika familia ya kishua. Kasota sana kabla hajafika hapo alipo. Kitendo cha kutoka  na kuwa karibu na msanii mwenye vision pana kama Diamond ni wazi Harmonize asingeweza kudumu na msichana mwenye maisha ya sinema kama Wolper.

Ilionekana mapema wao kutodumu pamoja. Kutengana kwao kama kweli kupo basi siyo habari kubwa sana, ilikuwa ni suala la muda tu.

Ila nilitamani kabla hawajaingia katika mahusiano yao ya kimapenzi  wangeonana na H. Baba na Flora Mvungi  na kupata ‘uchawi’ wa mahusiano yao.

Zamani H. Baba aliwahi kuwa katika mahusiano na Irene Uwoya. Wengi waliona kuwa mahusiano yale yalikuwa maigizo tu. Ni kipindi ambacho Uwoya alikuwa juu sana katika filamu huku H. Baba akiwa Mfalme mpya wa TAKEU baada ya Mr Nice hesabu zake kukataa.

Kama ilivyo ada kuwa ukweli huwezi kuwa uongo, muda si mrefu wawili hao wakaingia katika mtafaruku uliozaa matusi, kashfa na kudhalilishana. Hatimaye penzi la H. Baba na Uwoya likafa kibudu.

Ila baada ya miaka kadhaa, H. Baba akaonekana kunata kwa Flora Mvungi. Flora ni tofauti na wasanii wengi wa kike. Flora huwa hajisifii ujinga, haishi kimaigizo na ni mtu wa kazi tu kwa wanaomfahamu.

Kitendo cha kusikia H. Baba anatoka kimapenzi na Flora, wengi walijua ni mapenzi halisi. Ukweli daima hubaki ukweli. Flora na H. Baba wakaoana na sasa wana familia yao.

Wito wangu kwa Wolper na wengine wenye kariba kama yake ni kwamba ujana una mwisho. Na kabla ujana haujafika mwisho ni vema wakafahamu kuwa kama ilivyokuwa wakati wa amani ndiko kunakotengenezwa silaha, basi ni wakati wa ujana pia ndiko kwenye maandalizi madhubuti  ya familia na maisha ya uzee.

Wolper amevuka katika miaka ya ukuaji. Sasa kama mtu makini na mwenye uono wa mbali hapaswi kuyumbishwa na ustaa wake ama picha anayoiona akijitazama katika kioo.

Kila siku kubadili wapenzi tena katika namna ya fedheha na kuanikana katika mitandao ya kijamii hakimuongezi kitu zaidi ya kumshushia heshima na thamani. Kwanini hajui kuwa moja ya kitu kinachomshushia  mwanamke heshima  ni kuonekana  kutoka na wanaume wengi?

Sifa za kutamba katika mitandao na magazeti kwa sababu ya kubadili wanaume ilikuwa ni sifa ya zamani. Sasa siyo sifa tena bali ni fedheha na matusi.

Natamani kabla Wolper na Harmonize hajawaingia katika kile walichoamua wao kukiita mapenzi wangemuona H. Baba na Flora kisha wawaulize, kwani wenzetu nyinyi ilikuaje mpaka mmedumu mpaka leo? Nawasilisha!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles