31.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

NASTY C AJIACHIA NA 50 CENT

NEW YORK, MAREKANI


RAPA kutoka nchini Afrika Kusini, Nsikayesizwe Junior Ngcobo maarufu kwa jina la Nasty C, ameonekana akiwa nyumbani kwa rapa 50 Cent, jijini New York nchini Marekani.

Msanii huyo inasemekana yupo nchini Marekani kwa ajili ya kuzidi kuitangaza albamu yake ya Strings and Blings, hivyo kuonekana akiwa na 50 Cent kunaweza kumletea mafanikio zaidi.

Picha hiyo imesambaa kwenye mitandao mbalimbali nchini Afrika Kusini, hivyo mashabiki wana imani kuwa rapa huyo hawezi kutoka hivi hivi bila ya kufanya kitu na mkongwe huyo wa muziki duniani.

Nasty C, aliwahi kutwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop katika  Tuzo za Freshman Award mwaka 2015 na kuwa msanii mwenye umri mdogo kuchukua tuzo hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,507FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles