27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MTIKISIKO, HAMAHAMA WAPINZANI YAFIKA 143

Na AGATHA CHARLES             |                


TANGU vuguvugu la madiwani na wabunge wa vyama vya upinzani, hasa vya Chadema na CUF kujiuzulu na kuhamia CCM lianze mwaka juzi, imebainika idadi yao sasa imefikia 138.

Vitendo vya madiwani na wabunge wa vyama hivyo kuhama, vimeendelea kuchukua sura mpya siku hadi siku na hadi sasa idadi ya madiwani wa Chadema waliojiondoa na kujiunga CCM imefikia 129 huku CUF ikifikia tisa.

Taarifa ambayo MTANZANIA Jumapili imeipata wiki hii kutoka Kitengo cha Habari cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilieleza katika uchaguzi mdogo ujao utakaofanyika Septemba 16, unaojumlisha kata 23 Tanzania Bara, Chadema kina kata 15 za madiwani waliojiuzulu, akiwamo Diwani wa Monduli Mjini ambaye pia alikuwa ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Isack Joseph maarufu kwa jina la Kadogoo.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikuwa na idadi ya madiwani waliojiuzulu na kusababisha uchaguzi wa mdogo uliofanyika Agosti 12, mwaka huu ukijumlisha kata 36 kutoka kata 77 zilizotangazwa awali baada ya madiwani 41 kupita bila kupingwa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji, alisema katika uchaguzi huo, idadi ya madiwani wao waliojiuzulu na kujiunga CCM walikuwa 54.

Kwa upande wa CUF, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi (kambi ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad), Mbarala Maharagande, aliliambia gazeti hili hadi sasa idadi ya madiwani wao waliohama imefikia tisa.

Alisema hakuwapo ofisini kuweza kupata majina ya madiwani hao na kata zao, lakini walitoka Tanga, Mtwara, Dar es Salaam, Kondoa na Nachingwea.

Jana gazeti moja la kila siku liliandika kuwa juzi pekee kulikuwa na madiwani saba kutoka kata za mkoani Pwani waliohamia CCM wakitokea vyama vya upinzani.

Gazeti hilo liliwataja majina na kata zao katika mabano kuwa ni Ally Mbwana (Ikwiriri), Abdul Omari (Kisiju), Sultan Waziri (Njia nne), Issa Salum (Magindu), Shabashaba (Ruvu), Hassan Mohamed  na Hamis Mbonde.

Pia idadi aliyoitaja Maharagande inamjumuisha aliyekuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mussa Kafana, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwalani, aliyejiuzulu juzi na kuomba kupokewa CCM.

Kafana alipishana siku kadhaa na aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia alikuwa Diwani wa Kata ya Vingunguti (CUF), Omary Kumbilamoto, aliyehamia CCM mwezi uliopita.

Awali kabla ya taarifa hizo mpya, Februari, mwaka huu gazeti hili liliandika kuwa hadi wakati huo madiwani 60 wa Chadema walijiuzulu nyadhifa zao na kujiunga na CCM.

Sababu za madiwani hao kujiondoa Chadema hazitofautiani kwa sababu wamekuwa wakitoa hoja kuwa wanahamia CCM kuunga mkono utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli.

Hadi sasa imebainika kuwa Mkoa wa Arusha ndio unaongoza kwa idadi kubwa ya kata zake kuondokewa na madiwani, huku Halmashauri ya Monduli pekee madiwani wake wanane walijiuzulu na kujiunga CCM.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles