31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NASSARI: TAREHE YA KWENYE VIDEO NI ‘SETTING’

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ametoa ufafanuzi kuhusu tarehe ya picha inayoonekana kwenye video aliyoitoa kama ushahidi wa jinsi wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanavyoshawishiwa kwa rushwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.

Katika video hiyo Nassari aliyoionyesha na kuwakabidhi waandishi wa habari mjini Arusha jana, tarehe inasoma ilichukuliwa Januari Mosi, mwaka 2008.

“Ile tarehe ni ya kiwandani ni tatizo la ‘settings’ mipangilio, kwanza mwaka 2008 Mnyeti alikuwa anasoma mwaka wa pili Chuo Kikuu cha St. Augustine lakini pia tujiulize mwaka 2008 wale madiwani walikuwa tayari madiwani,”

Aidha, Nassari amesema ni tatizo dogo linaeleweka ambapo amewataka watu kujikita kwenye matukio halisi ya kwenye video hiyo kuliko tarehe inayoonekana kwani hilo ni tatizo la kiufundi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles