28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

NAPE AISHAURI SERIKALI KUIMARISHA MIPAKA

Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Nape Nnauye ameishauri Serikali kuboresha mipaka ya nchi kwa wakati ili kuondokana na migogoro inayojitokeza mara kwa mara.

Nape amesema hayo leo katika ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Mazingira ilipotembea mipaka kati ya Tanzania na Uganda Wilaya ya Missenyi upande wa Tanzania Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Isingiro upande wa Uganda.

Amesema suala la kulinda mipaka ni muhimu hivyo ni vyema serikali kupitia Wizara ya Ardhi ikatenga fedha za kutengeneza barabara zilizoko mipakani ili kurahisisha ulinzi na usalama wa mipaka yetu na kuwezesha wakazi wa nchi hizi mbili kutambua mipaka ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi.

“Tumebaini kuwa kuingia kwa wananchi wa Uganda hasa kuleta mifugo yao katika ranchi ya Missenyi kunachangiwa na kutokuwapo njia na alama maalumu zinazotenganisha kati ya nchi na nchi hivyo watu wanaingia kupitia katika vichochoro visivyo rasmi na kuhatarisha amani kwa wakazi wa mipakani,” amesema.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula amesema kuwa hadi sasa Wizara imepokea Sh bilioni nne za kuimarisha mipaka ambapo fedha zitakazotumika kuimarisha mpaka wa Tanzania na Uganda ni Sh bilioni 1.9 na Sh bilioni 2.1 kwa mpaka wa Tanzania na Kenya.

“Kuna watu waliomba maeneo wakafuge lakini wameshindwa na baadhi wanayatumia kwa kazi ambazo hazieleweki huku baadhi wakiomba kufugia lakini wanayatumia kwa ajili ya kazi nyingine, nitawachulia hatua kama watashindwa kufanya kazi waliyoomba alisema Mabula,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles