NA CHRISTOPHER MSEKENA
THE African Princess, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema anaamini anayo nafasi nyingine kubwa zaidi ya kuvuna mafanikio ya kipaji chake cha muziki na kuiwakilisha vyema Tanzania.
Staa huyo ambaye mwaka huu amechomoza kwenye tuzo kubwa za Afrima, amesema muziki siyo kuimba, kuna vitu vingine vya ziada ambavyo humpa msanii nafasi ya kupaa juu zaidi kwenye tasnia.
“Namshukuru sana mwenyenzi Mungu kwa kila kibali anachonipa, naamini kwenye maandiko yake huu ni mwaka wa kupaa juu kama zaidi kama Tai,” alisema Nandy anayetamba na ngoma yake ya Wasikudanganye.