26.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

NAKUMAT ARUSHA YAPIGWA KUFULI

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

 

CHAMA cha Wakulima Tanganyika (TFA), kimelifunga duka kubwa la NAKUMAT tawi la Arusha kwa kushindwa kulipia kodi ya pango.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa duka hilo zinadai kwamba kufugwa kwa duka hilo kunatokana na mwekezaji huyo kudaiwa zaidi ya Sh milioni 300 za kodi ya pango.

 

Mhasibu Mkuu wa TFA Arusha, Evarist Kauki jana alilithibitishia gazeti hili kufungwa kwa duka hilo kwa sababu ya kushindwa kulipa kodi.

“Ni kweli kama unavyoona sisi wamiliki wa jengo hili TFA tumelazimika kufunga duka hili kwa sababu wateja wetu hawajatulipa kodi ya pango kwa muda mrefu sasa.

 

“Siwezi kukutajia kiasi gani tunawadai kwa sababu mkataba wetu ni siri. Hatua hii hatujakurupuka, tulitoa taarifa ya siku 30 kwa wateja wetu wakanyamaza bila kujibu.

“Sasa baada ya hapo kilichofuata ni kufunga duka na ikipita siku 14 kama watakuwa hawajalipa fedha tunazowadai basi tutalizimika kupiga mnada vitu vilivyopo ndani kwa mujibu wa sheria na mkataba wetu,” alisema Kauki.

 

Baadhi ya wafanyakazi wa NAKUMAT waliokutwa na gazeti hili nje ya duka hilo walieleza kuwa mwajiri wao hapaleki makato ya fedha za mfuko wa hifadhi ya jamii.

 

Kiongozi wa wafanyakazi aliyejitambulisha kwa jina la Neema Siwa alithibitisha mamdai ya wafanyakazi kuwa mwajiri hawasilishi michango ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

 

“Kuna wafanyakazi wana madai mengi sana hapa ya likizo, wengine mishahara hawajalipwa. Lakini baya ni kwamba fedha zetu za NSSF hazijapelekwa kwa muda mrefu.

 

“Hali hii ni kama wawekezaji wanaijua kwa sababu wamekuwa nje ya Arusha kipindi kirefu sana bila kutoa ufafanuzi kwa wafanyakazi licha ya juhudi za kufuatilia mara kwa mara tulizozifanya,” alisema Siwa.

 

 

Alipoulizwa Meneja wa NAKUMAT Tanzania, Alfrick Milimo kuhusu kufungwa kwa duka hilo alisema wako katika mazungumzo na mwenye jingo lakini wanakabiliwa na ukata.

 

“Mzunguko mdogo wa fedha umesababisha tushindwe kumudu kulipa gharama za kodi za majengo. Suala la Arusha bado tunaendelea na mazungumzo kati yetu na uongozi wa Nairobi, Kenya na TFA,” alisema Milimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles