24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mwinyi Zahera aukomalia ubingwa ligi kuu Bara

TIMA SIKILO- DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema pamoja na changamoto wanazopitia, bado wanaufikiria ubingwa na wanapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika kila mchezo.

Yanga juzi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Alliance FC mkoani Mwanza.

Timu hiyo inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 64, baada ya kucheza michezo 26, ikishinda 20, sare nne na kupoteza michezo miwili.

Akizungumza alipotembelea ofisi za gazeti hili zilizopo Sinza Kijiweni, Dar es Salaam jana, Zahera alisema awali alikuwa haufikirii ubingwa kutokana na aina ya kikosi alichonacho, lakini baada ya kuzisoma timu zote anaamini timu yake ina nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa huo.

Zahera alisema katika timu zote za ligi ambazo amecheza nazo ana imani hakuna ambayo inaweza kumkwamisha, japokuwa zipo ambazo walikosa matokeo na hiyo ni kutokana na maamuzi mabovu ya waamuzi na si kiwango kibovu cha wachezaji wake.

“Nimeziangalia timu zote, kasoro Azam pekee, ambayo bado nina imani kubwa timu yangu ina nafasi ya kuutwaa ubingwa wa ligi kwa msimu huu na hata misimu ijayo endapo mipango itakwenda kama tulivyopanga,” alisema.

Aidha, Zahera alisema anawaomba mashabiki kuisapoti timu yao kwa kuchangia michango mbalimbali, ili kuiwezesha timu kufikia malengo kwa misimu ijayo.

@@@@@@@@@@@ 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles