22.1 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenezi CCM Ileje agawa bendera kwa mabalozi 21 tawi la Isongole

Na Denis Sinkonde, Songwe

Katika kuendelea kukijenga Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Katibu Mwenezi wa chama hicho, Maoni Mbuba amekutana na kugawa bendera kwa Mabalozi Tawi la Isongole ikiwa ni hatua ya kujipanga kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.

Mbuba amekutana na mabalozi hao Julai 12, 2023 katika ofisi za Tawi la CCM, Isongole ambapo amewasihi mabalozi hao kupendana ndani ya Chama na kujiepusha na makundi ambayo yanaweza sababisha kupoteza ushindi kwenye chaguzi zijazo.

Mbuba amewakumbusha mabalozi hao umuhimu wao ikiwemo kuandaa viongozi wa Serikali na Chama hivyo wanapaswa kutambua mamluki ndani ya chama na kuwasilisha kwa viongozi wao ili wasaliti wote wachukuliwe hatua za kindidhamu wakiwepo wanaobeza shughuli zinazosimamiwa na serikali ya CCM.

“Nimewagawia bendera hizi baada ya kutambua umuhimu wenu ndani ya chama hivyo zipeperusheni ili chama kionekane kipo hai huku mkiendelea kukijenga chama kuanzia ngazi ya shina mpaka wilaya.

“Kama mwenezi wa wilaya ya Ileje ninatarajia kuanza ziara ya kutembelea halmashauri kuu ngazi ya matawi wilaya yote kwa lengo la kueleza matarajio ya chama na kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu sambamba na kuwahamasisha kujisajili na kulipia kadi za uanachama kwa muda muafaka,” ameeleza Mbuba.

Katibu wa CCM kata ya Isongole, Obeid Mwambene amewapongeza mabalozi hao namna wanavyofanya kazi za kukijenga chama nakuwaahidi kama chama kitawapa ushirikiano Kwa lengo la kwenda kwenye uchaguzi mkuu na serikali za mitaaa.

Mwenyekiti wa tawi la Isongole kata ya Isongole, Samsoni Msongole amewataka mabalozi kuwa na orodha kamili ya wanachama Walio hai Kwa lengo la kujipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu 2025 kupata viongozi watakaoleta maendeleo ya wananchi.

Mmoja wa mabalozi hao, Osca Mbwile amesema changamoto inayowakabili kama mabalozi ni pamoja na kuwa na wanachama wasiokuwa na kadi kutokana na baadhi yao kulipia kadi bila kupewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles