23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mwendokasi wasababisha kifo cha diwani Singida

Na Seif Takaza, Iramba

Watu watanio akiwamo Diwani wa Viti maalumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Wanjuka Mkumbo wamefariki dunia kufuatia ajali iliyosababishwa na basi la Tanzanite, Agosti 17, mwaka huu lenye namba za usajili T 916 BNU.

Akizungumza juzi katika mazishi ya Wanjiku, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake mkoani Singida, Prisca Maleta amesema kuwa yeye alishuhudia ajali hiyo mwanzo hadi mwisho.

Prisca amesema kuwa wakati basi hilo linapinduka yeye na watoto wake walishuhudia na kutoa msaada kwa marehemu Winjuka ambapo alimweleza kwamba toka basi hilo litoke Singida lilikuwa katika mwendokasi.

“Mimi nilifuatilia tukio hilo nilipokuwa naongea na Winjuka eneo la ajali aliniambia kwamba basi hilo lilikuwa na mwendo kasi na walipofika Manyoni abiria walimkataa dereva aliyekuwa akiendesha basi hilo akaingia dereva mwingine, hata hivyo dereva aliyebadilishwa akawa ana mwendokasi zaidi ndio hali iliyopelekea wakapata ajali hiyo,” amesema shuhuda huyo kwa masikitiko.

Shuhuda huyo alisema yeye aliyekuwa akiishuhudia ajali hiyo akiwa katika gari jingine lililokuwa nyuma ya basi lililopata ajali ambapo aliona jinsi gari hilo lilivyokuwa linapinduka.

Shuhuda huyo alifanikiwa kutoa msaada kwa majeruhi kadhaa wa basi hilo akiwemo marehemu Winjuka kabla hajafariki ambapo alimfahamisha juu ya yaliyojiri kabla ya ajali kutokea na kumpa taarifa zake binafsi kuwa yeye ni diwani wa halmshauri ya wilaya ya Iramba ambapo ilirahisisha kuwafahamisha ndugu wa Diwani huyo.

“Tunaiomba Serikali iangalie kwa makini wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na madereva wao wanaoendesha vyombo hivyo kuwa makini kwani wao wanabeba roho za watu wanapokuwa safarini hivyo wanapaswa kufuata sheria za usalama barabarani.

“Jambo la pili tunaiomba jamii inaposhuhudia matukio ya ajali inabidi kuwasaidia majeluhi na kuwapeleka hospital au vituo vya afya lakini cha kusikitisha kwa macho yangu nimeona vijana wakipora mali za majeruhi na wale waliopoteza maisha pamoja na kuwasachi mifukoni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga vituo vya afya, zahanati na hospitail lengo likiwa kuwasaidia wananchi pale wanapokuwa wagonjwa na wengine kupata ajali lakani amesikitishwa na kitendo cha majeruhi wa ajali hiyo kuona wakipoteza maisha licha ya kuwepo kwa hospitali karibu na eneo la ajali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles