30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Mwasisi wa Msondo, Kapteni John Simon aaga dunia

Kapten aliyefarikiNA JIMMY CHIKA

MWANAMUZIKI mkongwe, Kapteni John Simon, ambaye ni mmoja kati ya wanamuziki walioanzisha bendi ya NUTA Jazz Msondo Ngoma mwaka 1964, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata), Hassan Msumari, mkongwe huyo alifariki Jumatatu katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa moyo.

Kiongozi wa bendi ya Shikamoo Jazz aliyokuwa akiitumikia hadi mwisho wa maisha yake, Ally Adinani, alisema mazishi ya mwanamuziki huyo yatafanyika leo katika makaburi ya Karakata, jijini Dar es Salaam.

Mwanamuziki huyo alizaliwa mwaka 1940 na alianza kuimba mwaka 1954 akiwa na bendi mbalimbali, ikiwemo Kigogo Jazz, Western Jazz na kisha mwaka 1964 akajiunga na bendi ya Msondo Ngoma.

Huko alifanya kazi na marehemu Muhidin Gurumo, mpiga solo raia wa Zaire, sasa DRC, Hamisi Franco, Kiiza Hussein, Mabruok Khalfan na Ahmad Omar, ambapo kwa sasa waasisi wote hao wameshafariki dunia.

Baadaye kwenye miaka ya 1970 John Simon alihamia bendi ya JKT Stereo, ambapo alikuwa kiongozi, alishiriki kutunga wimbo wa ‘Majambazi’, ‘Mtoto Yatima’ na nyingine nyingi.

Alipoachana na bendi hiyo mwaka 1994 alikuwa ni mmoja kati ya wanamuziki wakongwe walioanzisha bendi ya Shikamoo Jazz, ambayo aliitumikia hadi mwisho wa maisha yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles