27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanza yajitungia mtihani wake wa taifa

BENJAMIN MASESE-MWANZA

Siku chache baada ya Serikali mkoani Mwanza kuweka maazimio 14 kwa  walimu wakuu, maofisa  elimu wa kata na taaluma ili kuinua ufaulu kwa shule za msingi 2019/2020, imeanza kutekeleza kwa vitendo kwa wanafunzi wa darasa la saba wanaotarajia kufanya mtihani wa taifa katia ya Septemba 11-12, mwaka huu.

Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Michael Ligola kwa kushirikiana na maofisa elimu taaluma wa wilaya wamelazimika kutunga mtihani unaofanana na ule wa taifa na kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali katika kituo kimoja ili kujipima.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Ligola, Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mwanza, Longino Ludovick amesema lengo la Serikali ya mkoa ni  kuhamasisha, kuboresha taaluma na kuwaandaa wanafunzi   kuelekea mtihani wa taifa.

“Leo kama unavyoshuhudia  tumezikutanisha shule nne ambazo ni Butimba A na B, Bwiru na Gedeli ambazo zimetoka Ilemela na Jiji la Mwanza, hizi shule tumezikutanisha kwa sababu katika mtihani wa mock zilifanya vizuri hivyo tunataka kuona ipi inaongoza, shule itakayofaulisha wanafunzi wengi watapata zawadi ya pesa na mbuzi ya kwa ajili ya kitoweo cha mahafali,” amesema.

“Kwa wiki moja au mbili zilizobaki tutaendelea katika shule nyingine na changamoto zitakazojitokeza tutazifanyia kazi haraka kabla ya mtihani wa taifa, mitihani hii imetungwa na jopo la maofisa elimu kutoka mkoani na wilayani ndio maana unatuona hapa tukishughulika katika kituo hiki cha Shule ya Msingi Nyanza,”alisema.

Amesema  utaratibu  uliowekwa  katika mtihani  umezingatia masharti yote kama ilivyo ule wa taifa ambapo wanafunzi wa shule hizo walichanganywa  pamoja huku kila mmoja na dawati lake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles