29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka mwanafunzi

Beatrice Mosses, Manyara

Kijana mmoja aitwae Pascal Mananga (22), amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya sekondari Chief Dodo aliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Babati.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Simon Kobero aMEsema ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Hakimu Kobero ameieleza mahakama kuwa Machi 25 mwaka jana mwanafunzi aliyebakwa alimuaga mama yake anaenda kanisani na badala yake alikutana na kijana Pascal ambaye alimwambia aambatane nae hadi anapoishi kijana huyo ili ampe pesa kiasi cha Sh 10,000 akampe baba yake aliyekuwa akimdai na alipofika alimwambia kuwa hana pesa hiyo ndipo mwanafunzi akaendelea na safari yake kuelekea Kanisani.

Aliongeza kuwa wakati  mwanafunzi huyo anaelekea Kanisani kijana Pascal alikuwa akimfuatilia kwa nyuma na hadi kufika eneo hilo la korongoni kijana huyo akaanza kumshika akamdondosha chini na kumvua nguo na kuzitupa mbali na baadaye kumbaka.

Baada ya maelezo hayo hakimu aliuliza upande wa mashtaka kama wana chochote cha kueleza mahakama, ndipo Wakili wa serikali, Petro Ngassa akaiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili kutoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo  hivyo na hasa ikizingatiwa makosa kama hayo yamekuwa yakijirudia sana katika mkoa huo.

Baada ya ukimya huo Hakimu Kobero akamwambia mshtakiwa hana namna ya kumpunguzia adhabu hivyo utakwenda jela maisha na atachapwa viboko vinne pamoja na kutoa fidia kwa muathirika kiasi cha Sh milioni nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles