26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Serikali yatoa maelezo mapya vyeti feki

Mwandishi wetu-Dar es Salaam

 KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, amewataka wakuu wa taasisi  za umma na maofisa utumishi nchini kumaliza uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma vya ufaulu wa kidato cha nne, cha sita na ualimu.

Alisema ofisi yake imekuwa ikipokea taarifa za uwepo wa watumishi wachache wenye vyeti vya kughushi katika baadhi ya halmashauri na taasisi za umma.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na wizara hiyo jana, ilisema Dk. Ndumbaro alitoa maelekezo hayo ikiwa ni sehemu ya msisitizo wa utekelezaji wa maelekezo ya Rais John Magufuli aliyoyatoa wakati akizindua Bunge Novemba, 2015.

Rais Magufuli alielekeza utumishi wa umma nchini uwe wa uadilifu, unaowajibika na wenye sifa stahiki.

Katika taarifa yake ya jana, Dk. Ndumbaro amefafanua kuwa uwepo wa taarifa za watumishi wenye vyeti vya kughusi hadi sasa unaashiria kuwa kuna baadhi ya wakuu wa taasisi na maafisa utumishi hawajalipa uzito unaostahili zoezi la kuwaondoa watumishi wenye vyeti vya kughushi.

“Mpaka sasa bado tunapata taarifa za baadhi ya watumishi wenye vyeti vya kughushi kuendelea na utumishi wa umma katika baadhi ya halmashauri na taasisi, hivyo inatulazimu kuwasilisha vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki badala ya kuendelea na utekelezaji wa majukumu mengine ya kitaifa,” alisema Dk. Ndumbaro.

Katika hatua nyingine, Dk. Ndumbaro aliwataka watumishi wa umma nchini kuwajibika kwa Serikali na wananchi pindi wanapofuata huduma katika taasisi zao ili kujenga mahusiano mazuri kati ya Serikali na wananchi.

Dk. Ndumbaro alitoa wito kwa wakuu wa taasisi kuhakikisha wanasimamia nidhamu mahala pa kazi ili watumishi wa umma waweze kutumia muda wao wa kazi vizuri kwa kutoa huduma bora kwa umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles