30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Mwanri aonya watakaorudi shuleni na mimba

 ALLAN VICENT– TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanatulia nyumbani hawajihusishi na vitendo vya ngono katika kipindi hiki ambacho Serikali imefunga shule na vyuo ili kuwaepusha na maambukizi ya virusi vya corona.

Alitoa onyo hilo jana katika mdahalo maalumu wa wadau wa maendeleo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Afya Tabora na kurushwa mubashara kupitia vituo ya redio na mitandao ya kijamii mkoani hapa.

Alisema baadhi ya wazazi na walezi wameacha watoto wao wakizurura ovyo mitaani badala ya kuwasaidia watulie nyumbani na kujisomea kinyume hatua inayosababisha baadhi yao kujiingiza katika vitendo vya ngono na michezo mingine isiyofaa.

Mwanri alitahadharisha kuwa mtoto yeyote atakayerudi shuleni na mimba atachukuliwa hatua yeye na wazazi wake.

“Shule zitakapofunguliwa kazi ya kwanza tutakayofanya ni kuwapima watoto wa shule zote, yeyote atakayekutwa na ujauzito atachukuliwa hatua yeye na mzazi au mlezi wake,” alisema Mwanri.

Alimtaka Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk. Honoratha Rutatinisibwa, kwa kushirikiana na waganga wakuu wa wilaya zote kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa ipasavyo na mwanafunzi yeyote atakayekutwa na ujauzito hatua kali zichukuliwe haraka iwezekanavyo.

Aidha aliwataka viongozi wa vitongoji na watendaji wote wa vijiji na kata kuelimisha wazazi na walezi ili wakae vizuri na watoto wao katika katika kipindi hiki ili kuwaepusha na maambukizi ya corona na mimba za utotoni.

Awali Mratibu wa Wajasiriamali wa Mkoa huo, Asha Mwazembe, aliwataka wazazi na walezi kuwachunga watoto wao katika kipindi hiki cha mapumziko ya dharura kabla shule hazijafunguliwa.

Alisema baadhi ya wanafunzi wameachwa huru hawasomi wamekuwa wakizurura ovyo mitaani badala ya kukaa nyumbani na kujisomea.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles