23.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAMITINDO CALISAH USIHARIBU SIFA YAKO KWA JAMII

NA CHRISTOPHER MSEKENA

UKITAJA orodha ya wanamitindo wa kiume wenye miili iliyojengeka vyema kiasi cha kuzivutia kampuni mbalimbali kuwekeza fedha zao, jina la Calisah ni lazima liwepo, kwa kuwa ni modo mwenye viwango vya ubora nchini.

Calisah, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa baada ya uhusiano wake wa kimapenzi na Wema Sepetu kuvuja, ni modo mwenye malengo na ana kasi ya kufukuzia ndoto zake za kuwa modo mkubwa duniani kutoka Bongo.

Mara ya mwisho kuongea naye alikuwa tayari ameanza michakato ya kuhakikisha anatanua wigo wa kazi zake, ikiwamo biashara ya kukodisha warembo (video vixen), sehemu (location) na magari ya kifahari kwa ajili ya wasanii wa muziki wanaohitaji, hivyo hivyo kwenye video zao.

Modo huyo, ambaye ni bosi wa kampuni ya 0 + Limited, inayofanya shughuli za kukodisha warembo na magari ya kifahari kwa wanamuziki, wiki hii amezua taharuki kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha ya bidhaa mpya ya kike anayoitangaza.

Bila shaka Calisah yupo kazini, amevuta mkwanja mrefu wa kutangaza viatu vya kike (high heels), ambapo kwenye kurasa zake mitandaoni aliweka picha akiwa amevaa viatu hivyo.

Hali hiyo imepokewa kwa namna tofauti na mashabiki wa burudani nchini, wapo waliomwelewa kuwa lengo lake ni kutangaza bidhaa hiyo ya kiatu cha kike na wapo ambao hawakumwelewa, hasa ukizingatia Calisah ni modo wa kiume.

Kwa mtanzamo wangu, naliona tatizo hapo, hivi kwani ni lazima modo wa kiume atangaze bidhaa za kike? Hakuna mamodo wa kike wenye nguvu ya kutangaza bidhaa hiyo? Kama wapo, iweje Calisah akubali kuvivaa viatu vya kike kisa mkwanja?

Nafahamu kuwa Calisah yupo kazini na kinachoangaliwa ni fedha tu, bila kujali madhara ambayo yanaweza kutokea baada ya watu kutia shaka, uhalali wa modo huyo wa kiume kuvitinga viatu vya kike.

Lengo la dili hilo limekamilika kikamilifu na Calisah amefanikiwa kuvitangaza viatu hivyo kwa kiasi kikubwa, japokuwa dili hilo limeiharibu taswira yake, hasa ukizingatia yeye ni mtoto wa kiume.

Anafanya watu wamfikirie tofauti, anajitengenezea picha mbaya na inawezekana hapo baadaye ikaja kumkosesha dili nyingine za fedha ndefu kwa kuwa leo ameamua kuwachefua mashabiki wake. Lazima tukubali kufanya kazi zitakazolinda majina yetu kwa faida ya baadaye.

NUKUU

“Tunaowaita Role Models nao wana vitu ambavyo hatupaswi kabisa kuviiga kutoka kwao, tuchukue vinavyopendezea jamii zetu, vingine tuwaachie wenyewe.” Manii Mwasiti.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles