23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

MV Logos Hope: Meli ya Maktaba inayotembea

MELI

Na FARAJA MASINDE,

NI meli pekee duniani ambayo imebeba vitabu zaidi ya 5,000 pamoja na video, huhudumu kama maktaba, mapema mwaka 2016 ilitia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.

Meli hiyo inamilikiwa na Shirika lisilo la Kijerumani la GBA (Gute Bucher fur Aller) ikiwa na maana ya Vitabu Vizuri kwa Wote.

Wananchi waliruhusiwa kuingia ndani ya meli hiyo kuanzia saa tatu na nusu asubuhi na saa 12 jioni ambapo ilikuwa kuanzia Jumanne hadi Jumamosi.

Jumapili ilikuwa inafunguliwa kati ya saa sita na nusu mchana mpaka saa 12 jioni ambapo siku ya Jumatatu ilikuwa haifunguliwi.

Ada ya kiingilio ilikuwa ni Sh 1,000 ambapo ili kuingia ndani ya meli hiyo ulitakiwa kuwa na kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria.

Nahodha wa meli hiyo ni anaitwa Durke, ambapo mbali na yeye kuna wahudumu wengine 400 kwenye meli hiyo ni ambao wanafanya kazi bila malipo.

Ilipotoka Dar es Salaam, MV Logos Hope, ilitarajiwa kuelea mjini Maputo, Msumbiji na baadaye Durban nchini Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles