27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

MUHIMBILI YAPATIWA MSAADA WA VIFAA TIBA

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Shirika la Australia Tanzania Society limeikabidhi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 25.

Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Chialo amekabidhi msaada huo leo Jumanne Machi 20, kwa Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH, Dk. Julieth Magandi.

Akizungumza baada ya kupokea amesema msaada huo unajumuisha vitanda vya wagonjwa, mashuka, ‘stand’ za kusimamishia dripu na viti maalum vya wagonjwa vifaa ambavyo vimekuja wakati mwafaka ambapo Muhimbili inaendelea kuboresha huduma zake.

“Tunashirikiana nao kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ikiwamo kutuunganisha na madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia na hivi karibuni ndani ya mwaka huu tutaanzisha kozi ya ‘plastic surgery’ katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas),” amesema.

Aidha, Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Chialo ameyashauri mashirika mengine kujitolea kwa jamii.

“Kutoa ni moyo, sisi tupo tayari kuendelea kujitolea kusaidia jamii, hivi tunavyoongea madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia wapo mkoani Mwanza ambapo watafanya upasuaji kwa watoto waliozaliwa na tatizo la mdomo sungura,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles