24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Mugabe ataka walioshiriki Olimpiki wafungwe

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe
RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe

HARARE, ZIMBABWE

RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amemuagiza Kamishna Mkuu wa Polisi nchini Zimbabwe, Augustine Chihuri, kuwakamata wanamichezo ambao walikwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil.

Rais huyo amedai kuwa wanamichezo hao lazima wakamatwe na kuwekwa ndani kutokana na kushindwa kurudi na medali katika michuano hiyo mikubwa ya kimataifa ambayo ilimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Zimbabwa ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zilishiriki michuano hiyo ya kimataifa na kushindwa kupata medali hata moja.

Washiriki kutoka nchini humo kwa upande wa riadha walikuwa 31, kati ya hao ambaye alifanya vizuri alishika nafasi ya 8.

Rais huyo amedai kutoridhishwa na matokeo ya wanamichezo hao na kudai kuwa walikwenda kufanya yao badala ya kupigania taifa kama ilivyo kwa mataifa mengine ya barani Afrika.

“Lazima wanariadha wote wakamatwe kwa kuwa hakuna ambacho wamekifanya kwa siku zote hizo nchini Brazil, kwa kifupi tumepoteza fedha za taifa kwa ajili ya panya hao ambao tunawaita wanariadha.

“Walikwenda na wakashindwa kujitoa kwa ajili ya taifa lao na wameshindwa kupata medali hata moja kati ya dhahabu, shaba na fedha. Kati ya wote 31 hakuna hata mmoja ambaye ameweza kushika nafasi ya 5 au 4, kama ilivyo kwa majirani zetu Botswana.

“Kwa nini walikwenda huko kwa ajili ya kupoteza fedha zetu, lazima wachukuliwe hatua kutokana na matokeo waliyoyapata,” alisema Mugabe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles