32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

Msaada zaidi waingia India wakati idadi ya vifo ikifikia rekodi mpya

Delhi, India

Msaada wa kimataifa wa kukabiliana na uhaba mkubwa wa hewa ya oksijeni nchini India umewasili katika taifa hilo la Asia Kusini jana, wakati idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona ikiongezeka na kufikia rekodi mpya.

Nchi hiyo yenye watu bilioni 1.3 iliripoti vifo vya watu 3,689 jana – huku kukiwa na visa vipya 400,000 vya maambukizi Covid-19. Marekani, Ujerumani, Urusi, Uingereza na Ufaransa ni miongoni mwa mataifa yaliyopeleka misaada ya dharura ikiwemo mitungi ya oksijeni, barakoa na dozi za chanjo.

Balozi wa Ujerumani nchini India, Walter Lindner, alisema baada ya mashine 120 za kusaidia kupumua kuwasili Jumamosi, kuwa wakati mwingine watu wanafariki nje ya hospitali kwa sababu hawana oksijeni na wengine wanafariki wakiwa kwenye magari yao. India imeutanua mpango wake wa utoaji chanjo kwa watu wazima, lakini majimbo mengi yanakabiliwa na uhaba wa dozi licha ya zuio la kuuza nje ya nchi kwa chanjo zinazotengenezwa nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles