29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

MKWASA ATAJWA KUTUA ZESCO, AZAM

KOCHA Boniface Mkwasa
KOCHA Boniface Mkwasa

Na MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

KOCHA Boniface Mkwasa aliyevunja mkataba wake jana na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, baada ya makubaliano kati yao ametajwa kutua katika klabu ya Zesco ya nchini Zambia na Azam FC.

Mkwasa aliyerithi mikoba ya Mholanzi, Mart Nooij, Julai 2015, mkataba wake wa miaka miwili ulikuwa unatarajiwa kuisha Machi mwaka huu na anatarajia kulipwa fedha zake ndani ya wiki hii kwa miezi iliyobaki.

Nafasi ya Mkwasa kwa sasa itarithiwa na Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga, atakayepewa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.

Habari kutoka ndani ya Zesco United zinaeleza kuwa Mkwasa ni kati ya makocha watatu waliopita katika mchujo baada ya klabu hiyo kubwa nchini Zambia, kutangaza nafasi ya kazi wiki iliyopita na makocha wengi kutuma maombi.

“Makocha watatu wanaowania kibarua Zesco ni Mkwasa, kocha wa zamani wa Simba Mcroatia, Zdravko Logarusic na Epraim Mashaba kutoka Afrika Kusini.

“Tulipokea maombi ya Mkwasa na wengine na amepita katika mchujo, sasa tunaangalia kati ya hao watatu waliobaki,” kilisema chanzo ndani ya Zesco.

Zesco iliamua kutangaza nafasi ya kazi baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, George Lwandamina ‘Chiken’, kujiunga na Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga.

Mbali na kuhusishwa na Zesco, Mkwasa pia anatajwa kutua Azam kama kocha msaidizi endapo dili la Mholanzi, Hans van der Pluijm, kutua kwa matajiri hao litakamilika.

Azam ambao wamewatimua makocha wao Wahispania wakiongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez, wanatajwa kuwa katika mazungumzo ya siri na Pluijm ambaye aliondolewa kwenye nafasi ya Kocha Mkuu Yanga na kumpisha Mzambia Lwandamina, huku yeye akipewa nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi katika klabu hiyo ambayo inadaiwa hana furaha nayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles