26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Mkuu NSSF afanya mazungumzo na taasisi tatu za kibenki nchini

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio, amefanya mazungumzo na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki nchini ambazo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kushirikiana katika nyanja mbalimbali.

Wakurugenzi wa taasisi hizo ambazo ni pamoja na NMB, CRDB  na UBA wamekutana leo Jumatano Septemba 19, jijini Dar es Salaam ambapo kwa pamoja wameazimia kuendeleza na kukuza mahusiano ya kibiashara.

Wakurugenzi hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Charles Kimei, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA, Usman Imam Isiaka na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker.

Aidha, mazungumzo katika mkutano masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao na NSSF yalizungumzwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles