23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mke wa Trump adaiwa kumuiga Michelle Obama

Donald Trump na Melania Trump
Donald Trump na Melania Trump

CLEVELAND, MAREKANI

SHEREHE ya ufunguzi wa kongamano kuu la wajumbe wa Chama cha Republican nchini Marekani, iligubikwa na utata wa hotuba iliyotolewa na mke wa mgombea urais wa chama hicho, Donald Trump.

Sehemu ya hotuba hiyo ya Melania Trump, inadaiwa kuigwa kutoka ile ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle, aliyoitoa miaka minane iliyopita.

Katika hotuba zote mbili, wawili hao wanajitambulisha kwa umma wa Wamarekani kwa kuzungumza misingi iliyoumba maisha yao.

Mke huyo wa Trump, ambaye ni mzaliwa wa Slovenia, amesema alipata usaidizi mdogo wakati wa kuandika hotuba hiyo, ambayo imesisitiza maadili ya kifamilia na kujumuishwa kwa watu wa matabaka yote.

Sehemu moja ya hotuba ya Melania ilisema: “Wazazi wangu walinifunza umuhimu wa kufanya bidii kutafuta unachotaka maishani; kwamba neno lako ndilo linaweka uhusiano na unapaswa kutenda kwa unachosema na kutimiza ahadi; kwamba lazima uwaheshimu watu.

“Na tunahitaji kupitisha somo hilo kwa vizazi vingi vijavyo. Kwa sababu tunataka watoto wetu katika taifa hili wajue kuwa kitu pekee kwa mafanikio yako ni nguvu ya ndoto zako na utashi wako wa kuzifanyia kazi.”

Katika hotuba yake, Michelle Obama alisema: “Mimi na Barack tulilelewa na maadili karibu sawa, kwamba unafanya bidii kutafuta unachotaka maishani; kwamba neno lako linaweka uhusiano na kwamba unafaa kutenda unachosema utatenda; kwamba lazima uwaheshimu watu, hata kama huwafahamu, na hata kama haukubaliani nao.

“Tumejenga maisha tukiongozwa na maadili haya na tutayapitisha kwa kizazi kijazo. Kwa sababu tunataka watoto wetu na watoto wote wa taifa hili — kufahamu kuwa kilele cha mafanikio yako ni kuzifikia ndoto zako na utashi wako wa kuzifanyia kazi.”

Mshauri Mwandamizi wa Mawasiliano wa Melania, Jason Miller, alitoa taarifa ambayo ilikwepa kuzungumzia suala la kuiga, lakini pia bila kulikana.

Hotuba hiyo ilishuhudia siku tata ya ufunguzi wa mkutano huo wa Republican, unaotarajia kumpitisha mumewe kuwa mgombea rasmi wa urais baadaye wiki hii.

Ni baada ya wajumbe wanaompinga Trump kuandamana na kulalamika baada kuzuiwa kuwasilisha pingamizi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles