NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAM
MIKOA mbalimbali nchini imetakiwa kutuma maombi zaidi kwa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, ili kufanikisha kufana kwa tamasha hilo mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, hadi sasa ni mikoa 17 imefanikiwa kutuma maombi hayo, ambapo idadi hiyo ni kubwa na haijawahi kutokea tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao, lakini bado tunahitaji mingine zaidi ijitokeze kwani tunachofanya kwenye kamati yangu ni kuendelea kupokea maoni kwa njia mbalimbali,” alisema Msama.
Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa, Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.