23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Migogoro ya kampuni itatatuliwa kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni- Prof. Mkumbo

Na Christina Galuhanga, Dar es Salaam

Migogoro ya kampuni itatuliwe kwa kufuata ya taratibu, sharia, kanuni na kama migogoro hiyo ipo mahakamani basi iachiwe mahakama kufanya maamuzi yake na sio kuingiliwa kwenye maamuzi hadi hapo itakapokamilika.

Kauli hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi ya Wakala wa Usajili wa Bishara na Leseni (Brela).

“Unaweza kukuta kwenye kampuni wamegombana kutokana na hisa au mmoja anataka kuzidisha hisa kwenye kampuni kinyemela, hayo yatatuliwe kisheria na kikanuni na sio kutumia busara sana ili kuweza kupunguza migogoro mingi,” amesema Prof . Mkumbo.

Prof. Mkumbo ametoa wito kwa wafanyabiashara kuwa na muamko wa kusajili biashara kwani kurasimisha biahsara kunaanza na kusajili, hivyo Watanzania na Wafanyabashara waitumie Brela katika kurasimisha biashara ili wapate faida za kutambulika wanapofanya biashara na kwamba taratibu za urasmishaji zimerahisishwa kwa njia ya mtandao.

Pia, Profe, Mkumbo amesema Brela imepewa jukumu la kuwezesha ufanyaji biashara nchini na sio kudhibiti biashara, hivyo katika utekelezaji wa majukumu amewaelekeza watumishi wa Brela kila wanapopokea taarifa kutoka kwa mfanyabiashara kutaka kufunga biashara au kampuni afuatiliwe kwa ukaribu kujua changamoto iliyopelekea kufikia hatua hiyo.

“Kama taasisi yenye jukumu kubwa tusione sifa kumhudumia mfanyabiashara anayetaka kufunga biashara labda ufungaji huo utokane na migogoro ndani ya kamopuni,” amesema Prof. Mkumbo.

Upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Godfrey Nyaisa amesema kuwa hadi sasa kwa mwaka huu wa fedha kampuni zilizosajiliwa ni 7,148 na malengo ya taasisi ni kufikia usajili wa kampuni 9,528 ambapo hadi sasa usajili umefikia asiliamia 75 ongezeko ambalo limetokana  na matokeo ya uboreshaji wa mifumo wa usajili kwa njia ya mtandao.

“Kwa sasa usajili wa kampuni nunakamilika ndani ya siku moja, changamoto hutokea endapo anayesajili amewasilisha nyaraka zenye kutiliwa shaka na wataalam wetu au kuwasilisha nyaraka zisizokamilika,” amesema Nyaisa.

‘Kama taasIsI yenye Jukumu kubwa tuslone sda kumbudurma mlanyaboshara anayetaka kufunga biashara labda ulungap huo utokane na migogoro ndani ya kampuni amesisitiza Mhe Mkumbo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles