25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mhadhiri aeleza chanzo cha mimba shuleni

Oscar Assenga -Tanga

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha St. Augustine cha jijini Mwanza , Judith Wander amesema sababu kubwa ya uwepo wa mimba kwa wanafunzi kwenye vyuo vikuu nchini ni kutokana na malezi mabaya waliyolelewa na jamii zao na hivyo wanapoyakosa wakiwa huko wanakuwa wapweke na kujikuta wakifikiria kulewa na hatimaye kutumbukia kwenye mahusiano na baadaye kupata ujauzito.

Wander aliyasema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili.

Alisema wanafunzi hao wakati wakisoma kwenye shule za sekondari unakuta wanapigiwa simu na baba zao, mama zao wanabembelezwa, lakini wanapofika vyuoni wanajikuta kama wapweke kutokana na mambo ya aina hiyo kutokufanyika kwao.

Wander alisema kwamba mambo hayo ndiyo chanzo cha mimba kwenye vyuo vikuu hali inayosababisha baadhi yao kujikuta wakishindwa kufikia ndoto zao za kupata elimu nzuri ambayo inaweza kuwasaidia kuwainua kimaisha wao na jamii zao kutokanaa na kufanya vitu ambavo sio vya msingi vilivyowapeleka huko.

Akieleza nini kifanyike kuondoa tatizo hilo, Wander alisema lazima vyuo vishirikiane na shule za sekondari kuwaandaa wanafunzi ili waweze kujua wanapokwenda vyuoni wanapaswa kufanya nini na hatimaye kuweza kuondokana na vitendo vya namna hiyo.

Akizungumzia suala la rushwa ya ngono vyuoni, alisema jambo hilo limekuzwa kwa sababu wakati mwengine kama wanafunzi wa kike hawataacha kutengeneza mazingira ya mwalimu kucheka naye mara kwa mara, kumsifia amependeza na mengineyo, hayo maneneo ya rushwa ya ngono watayasikia sana.

“Lakini kama una bidii darasani na kujituma, huna muda, wanafunzi wangekuwa ‘bize’, sidhani kama watakuwa na muda wa kufuatwa, acheni pia kuwatumia walimu ujumbe kwamba wamependeza,” alisema Wander.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles